Kutana na Maabara inayotembea nje ya uso wa dunia, ni ajabu na kweli



Alikua ni Rais wa 40 wa Marekani bwana Ronald Reagan ambae alikuja na aidia ya kuanzishwa kwa kituo cha anga ambacho kitakua nje ya uso wa dunia huku kikihusika zaidi na ukusanyaji taarifa mbali mbali juu ya mwenendo wa dunia, usalama wa mawasiliano ya ndani ya dunia na tafiti mbali mbali za nje ya dunia, hii ilikua mwaka 1980.
Wengi walimuona Rais Reagan kama kichaa, kwani ni jambo lisilofikirika, atimae mwaka 1998 ujenzi wa kituo kikubwa cha anga ukaanza kujengwa kwa kupelekwa baadhi ya vifaa maalum nje ya uso wa dunia, vifaa hivi vilikua vinapelekwa na ma rocket.
download (1)
Kituo icho kikubwa cha anga kinajulikana kama ISS yaani Internation Space Station, ndio kituo kikubwa kabisa cha masuala ya sayansi ambacho kiko nje ya uso wa dunia, kituo hichi kinaelea angani kama mwezi au nyota zilivyo, bila kushikiliwa na kitu chochote kile, na hakipotei au kuanguka kisha kutokomea kusikojulikana.
o-INTERNATIONAL-SPACE-STATION-facebook.jpg
zifuatazo ni dondoo kubwa zihusuzo kituo icho;
  • ujenzi wake ulianza rasmi mwaka 1998 na kukamilika mwaka 2012
  • Kinaendeshwa kwa mfumo wa GPS kufuata mzingo wake (orbit) na ndio maana hakijawai kupotea huko anga za mbali.
  • kinaizunguka dunia yote kwa dk.90 kwa spidi ya mita 17,500 kwa saa.
  • Umbali wake toka duniani mpaka kilipo ni maili 240.
  • ISS inatumia solar ili kupata nguvu ya kujiendesha,ambapo solar hizo hutegemea mwanga wa jua ili kupata joto na kulibadili joto hilo ktk mfumo wa umeme,kisha umeme huo huifadhiwa ktk battery tatu kubwa zijulikanazo kama nickel hydrogen battery,hizi hutumika kusambaza umeme hasa pale ISS inapokuwa imekingwa na dunia ama kivuli cha dunia kinakuwa kinapiga ISS hivyo kufanya mwanga wa jua kutokufika vyema.
 16938569907_90b5c8a831_o_0

  • kuna genereta iitwayo Solid fuel oxygen generator,hii hutumika pia kuzalisha oksijeni ndani ya ISS kwa kuunguza oxygen candles ambapo husababisha chemical reaction nakuzalisha oksijeni ndani ya kituo icho.
  • Wataalamu waliomo ndani ya kituo icho upelekewa chakula, maji na hewa toka huku duniani, vitu hivi uandaliwa na kusafirishwa na kampuni la NASA ambalo linaratibu karibu kila kitu toka kwenye icho kituo.
  • Kuna mtambo maalumu ambao unajiusisha na kubadilisha taka mwili kama hewa ya cabondioxide, mikojo na maji machafu ya wataalam walioko humo ndani ili kutumika tena (recycling).
  • Kuna mitambo ya ziada ambayo hutumia maji na gesi ya hydrogen kutengeneza gesi asilia ya oksijeni.
international-space-station-iss-551918

Comments

Popular posts from this blog

Je Uliwahi kuyajua mambo haya, Utastajaabu sana ukiyasoma